Wanawake hutumia miguu, nywele na sehemu zingine za mwili kuwasilisha hisia zao. Kati ya sababu kuu zinazowalizimu kutumia ishara katika mawasiliano ni vikwazo vya jamii ambavyo vinawazuia kuwatongoza wanaume. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwa bahati mbaya, baadhi ya wanaume ni mazuzu kwa kuelewa kina dada wanapotumia mbinu hii kuwaongelesha. Kulingana na mtaalam wa lugha ya ishara na mwandishi wa ‘The Body Language of Love’, Allan Pease, wanaume wanastahili kujua kutafsiri ishara hizi ili waongeze bahati zao za kujamiana.

Ikiwa ule mwanadada ambaye umekaa naye anashinda akiweka mguu juu ya mwingine na baada ya muda mfupi anatoa na kurudia ishara hii mara kadhaa kuna uwezakano utabahatika.

 Kwa upande mwingine, mwanamke ambaye hatingiki hata kidogo mukiwa pamoja hana mpango wa kukujua zaidi. Ni vyema uangalie hizi ishara ili usimalize mda wako kwa mtu asiyekupenda au uache dhahabu inayokutafuta ipite.

Kama mko kwa kikundi, wanawake pia wanatumia miguu kuonyesha ule mtu wamependa. Angalia mguu ule ambao uko juu ya mwingine umeelekezwa kwa nani kati yenu. Ikiwa ni wewe, kuna uwezekano umebarikiwa.

Kando na miguu, nywele ni kitu kingine ambacho kinawasaidia wanawake kuwasiliana. Msichana ambaye anacheza na nywele yake ikielekea upande wako amekupenda. Ni vyema pia ungalia mwelekeo wa kitendo hiki kwa makini. 

Kama kuna mtu mwingine ambaye ishara hii inaelekea kwake, tafuta msitu mbadala wa kuwinda.

#MyLifestyle