Kati ya mambo ambayo huudhi zaidi maishani mwa mwanamke ni kuwa na bwana mzembe kitandani. Binti anaweza pata kila kitu kwao ama ajitafutie isipokuwa ngono. Hiki ndicho kigezo muhimu sana wakati wawili huamua kufunga pingu za maisha. Kila binti anashauriwa aangalie vitu hivi kama hataki kuwa na mume kama jina bila vitendo:

Share news tips with us here at Hivisasa

Hana maono

Mwanamume ambaye hajui anataka kufanya nini mwaka ujao na hana mipango ya siku za usoni kwa ujumla ni gogo lisilostahili kupendwa. Kama hawezi kupanga maisha yake, ni hakika kuwa hatajitayarisha kukufurahisha kitandani.

Hafanyi mazoezi

Hii shughuli muhimu ya ndoani hutaka mtu mwenye afya nzuri. Mojawapo ya njia za kuwa na afya njema ni kufanya mazoezi. Ikiwa mchumbao anashinda kwa nyumba na kula matunda na sharubati toka jokovuni, huyo ni mnyonge.

Hajui kupiga busu

Busu ni sura ya kwanza ya riwaya ya mapenzi. Yeyote ambaye ananakili uzembe na kutojua katika sura hii hastahili kupewa nafasi ya kuendeleza riwaya ya upendo. Chunga sana kama mume hakupi muda wa kuhisi uzuri wa busu kwa kupapia sehemu zingine bila matayarisho.

Hasifu maumbile yako

Kujamiana huanzia akilini na maumbile yako ni kiungo muhimu sana katika upishi huu wa kitandani. Kama hamiminii sifa makalio yako, pua, macho ama uso na viungo vinginevyo, kumpa tunda lako utakuwa msaada usiofaa. 

Kila mnapojamiana utakuwa unatafuta sababu yake ya kulala nawe ikiwa hajawahi kueleza jinsi urembo wako unamzingua. Hili litafanya usitosheka hata kama si mzembe katika sekta hii. 

Aidha, kuna uwezekano hatakufanyia jinsi angemfanyia yule anayesifu urembo wake.

#MyLifestyle