Mafuta ya nazi ni zawadi asili ambayo kila binti wa Mombasani anastahili kuanza kutumia. Wale ambao wametambua umuhimu wa haya mafuta wanayatumia sehemu mbalimbali zikiwemo zile za siri. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Urembo wa kuvutia unapatikana mnazini. Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo vidosho wa Pwani wanawezatumia nazi:

Saratani ni gonjwa hatari sana. Jinamizi hili limewamaliza wengi wakiwemo wanawake. Kwa bahati nzuri, wanawake wa Mombasa wanaweza kabiliana na ugonjwa huu wakitumia mafuta ya nazi. Kujipaka mafuta haya kwenye matiti kunapunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti ambayo inaua wanawake wengi.

Kukauka kwa sehemu kuu ya siri ya mwanamke ni hatari sana. Hali hii huwasumbua wanawake haswa wale ambao washapita umri wa kuzaa. Chanzo kikuu ni shida ya homoni ambazo hubadilika baada ya mke upitisha umri wa kupata watoto. Mafuta ya nazi yanaweza wasaidia wanawake kama hawa waendelee kufurahia ngono bila maumivu ama kutumia mafuta ya kulainisha yenye kemikali zinazoweza kudhuru afya yao.

Kando na sehemu za siri, mafuta haya yana matumizi mengi ya kiurembo. Kulainisha ngozi ni mojawapo ya wema wa nazi. Wapo wanaolinda nywele zao na wanaotoa vipodozi wakiyatumia. Vile vile, ukimuona msichana wa Mombasa ananengua kiuno akicheza mziki bila kuchoka, kuna uwezakano amekula nazi ambalo pia huondoa uchovu. Sifa hizi zinatulazimu tuulinde mumea huu.

#MyLifestyle