Mwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Kwale Zuleikha Juma Hassan amefichua kuwa mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa alimpigia simu Julai 8, na kumtishia.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye taarifa hapo Jumapili, Juma alifichua yafuatayo;

"Nataka kuwajulisha tu mujuwe kama kiongozi ninaye wakilisha wananchi wa Kwale. Mheshimiwa Aisha Jumwa amenipigia simu leo akisema yafuatayo:

1. Ananipa "warning" kwa sababu nilimtaja kwenye speech yangu wiki jana. (Nimemuambia kama nimemtaja anitumie hiyo video clip niione kama ushahidi wake)

2. Ameniambia nimuache na maamuzi ya kisiasa anayo fanya mimi hayanihusu. (Nimemuuliza aliemzuia nani?) 

3. Asema niwachane nae (mimi sijamtaja popote mbona ajishuku)

Mwisho nikamwambia simuogopi naogopa Mungu pekee mwenye nguvu za kupeana uhai na Mauti. 

Kando ya hivyo nimemuambia kama vile yeye ana haki ya kikatiba ya kuwa na msimamo wa kikatiba, pia mimi nina haki hiyo.

 Nauliza mbona kwa wenzangu misimamo ya kisiasa imekuwa personal au imekuwa kama vita vya kibinafsi? 

Mimi nashukuru sana mchango wa Mheshimiwa Raila Amollo Odinga katika siasa na maendeleo na haki zinazo patikana humu nchini, kwa mKwale, mpwani na mkenya kwa ujumla. 

Nani asiyejua kuwa wengi wa wanasiasa washupavu humu nchini wamekomaa kwa mafunzo yake.Mimi pia ninashukuru vile chama cha ODM kilivyo nipa mimi nafasi ya kujijenga kisiasa hadi sasa na pia nashukuru chama hicho na wote waliomo ndani kwa kuwa na misimamo inayo muinua mkono mlala hoi. Siwezi kukosa fadhila na siwezi toshiba ninyamaze malipo na dhulma.

Leo mkaazi wa Kwale siasa mbaya inaweza kufanya yeye akapokonywa ardhi zake na anaweza kukosa uhuru wake anaopata kupitia sheria tulizo pitisha za katiba yetu. Haya yote yanaweza kumdidimizwa zaidi ndani ya umaskini. 

Kama kiongozi wa Kwale lazima niwe na msimamo wa kisiasa ili kutetea maisha yetu na yale ya vizazi vijavyo. Siasa sio mchezo siasa ni maisha ya watu."

#hivisasaoriginal