Jahazi la ndoa linapoanza kuzama, watu wengi hulaumu wanawake bila kujua kwamba shida yaweza kuwa mume. Ikiwa watoto hawaonekani, mke ataitwa tasa bila kupata ushauri wa daktari. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Imani hii potovu inakulazimu wewe mke ufanye utafiti kudhibitisha ikiwa mumeo ana mbegu za kiume nzuri. Angalia sifa hizi kwa mwanamume:

1. Ujalivu

Ujalivu ni kunenepa kupita kiasi. Mwanamume aliyenenepa kupita kiasi ana uwezekano mkubwa wa kuwa mbegu za kiume chache. Ikiwa unampenda sana, itabidi umusaidie kupunguza uzito wake. Hili litasaidia mbegu zake za kiume zitembee kwa wepesi, kiasi cha mbegu hizi pia kitaongezeka na pia afya ya risasi hizi itaimarika.

2. Mazoezi na ulaji wa vitamini

Mazoezi ni mema kwa binadamu yeyote. Hakikisha mchumba wako anafanya mazoezi hata kama hajanenepa kupita kiasi. Mazoezi yatamsaidia awe na mbegu zenye afya ya kutamanika. Aidha, lazima awe mume wa kula vitamin kwa wingi. Vitamini CoQ10, E,C na D ni muhimu sana ukitaka kupata mimba.

3. Uraibu wa dawa za kulevya, pombe

Unashauriwa kutokubali waraibu wa madawa mbalimbali na vileo. Hawa wanaume watakupa kazi ngumu ndoani ukitafuta watoto. Hulka hii inawafanya wawe ni viwango vidogo vya mbegu za kiume.

Kwa sababu jamii inawatetea sana wanaume wakati ndoa inasambaratika, usifanye mzaha unapowinda baba wa wanao. 

Ikiwa umeoleka na Mungu hajawabariki na mtoto, elimisha mumeo kuhusu mbinu hizi na pia mtembelee daktari aliyehitimu.

#MyLifestyle