Caption-Chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Picha-Standard.

Chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa kinaajiri naibu chansela wa chuo hicho baada ya Josphat Mwatellah kufutwa kazi mwaka wa 2016.

Mahakama iliamuru kuwa haki za  Mwatella zilikiukwa na kuamuru alipwe shilingi milioni 28.

Laila Abubakar amekuwa akishikilia nafasi ya naibu chansella wa chuo hicho baada ya Mwatella kutimuliwa.

Kwa muda wa mwaka mmoja sasa Abubakar amekuwa akihudumu bila msaidizi wake kabla ya kuteuliwa kwa Joseph Rasowo.

Kati ya wakenya 14 waliotuma maombi yao ya kazi, ni 8 ambao wameitwa kufanyiwa mahojiano akiwemo Abubakar pamoja na naibu chansela wa chuo kikuu cha Taita Taveta.

Wengine ni Isaiah Omollo ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Kenyatta, Collins Ouma kutoka chuo kikuu cha Maseno miongoni mwa wengine.Mwenyekiti wa chuo hicho Kevit Desai ameiomba umma kutoa maoni yao kuhusu waliotuma maombi yao ya kazi.