Kuna wakati ambao wanaume hushindwa kuwaelewa wanawake wa pwani. Wanawake hawa hawapendi wanaume wa kucheza na nyoyo zao. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Hata yule mwanamke unayedhani hana roho ya kupenda, kuna mume mahali humzingua. Je? Ni nini siri ya mpenzi? 

Wanaume wengi wamebaki wakilaani baada ya kuachwa na wapenzi wao. Tatizo ni lipi? 

Sababu moja ya kuvunjika kwa uhusiano wa mapenzi ni kusahau majukumu yako. Leo tumekuletea siri nne za kuuteka moyo wa mwanamke.

1. Heshima

 Mke anastahili kuheshimiwa. Ukiheshimu mkeo, naye pia atafanya vivyo hivyo. La kusikitisha mno ni kwamba, kuna wanaume wamewadharau wanawake hadi wanawapiga mbele ya watoto. Hilo si jambo zuri.

2. Kuzingatia usafi

 Mwanaume lazima azingatie usafi. Mwanaume atamfurahisha mwanamke akiwa nadhifu. Jaribu uwezavyo uwe msafi kila wakati iwapo ungependa kumfurahisha mkeo.

3. Uaminifu 

Mume mwaminifu ni baraka kwa mkewe. Ndoto ya kila mwanamke ni kupata mume atakayemwamini. Ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya kukosa uaminifu.

4. Upendo wa dhati

 Ndoa yako haitadumu milele iwapo haina mapenzi. Ni jukumu la mume kumwonyesha mkewe anampenda kwa moyo wake wote. Kuna jinsi tofauti unaweza mwonyesha mkeo unampenda.

 Kwa mfano, mkeo atakupenda zaidi iwapo utamzawadi mara kwa mara. Kuna zawadi tofauti tofauti unaweza nunulia mkeo kama vile shanga, leso, mafuta ya kujipaka na kadhalika. Iwapo utaishi ukimzawadi mkeo, atazaidi kukupenda.

#hivisasaoriginal

#mylifestyle