Mombasa imejaa hekaya za mitaani na Magongo ina sehemu yake katika sekta hii. Ndugu wa toka nitoke wa Mogongo kitabia ni Mtwapa. Huku kumejaa majagina katika simulizi za Mombasani. Wazazi wa watoto ambao hawaishi huku wanawaonya wanao dhidi ya kuwa na marafiki kutoka sehemu hizi. Hulka ya huku inatisha kama nduli kwa wasiozoea hali hii.

Share news tips with us here at Hivisasa

Vituko vya Magongo vinafanana na hatari ambayo wacheza mpira wa magongo huwa ndani. Kama hauna vifaa vya kukuzuia, waweza vunjwa goti kwa rungu ama ung’olewe meno na mpira wenyewe.

Mtaa huu umejaa wezi na utingo ambao wanafahamu karibu kila sehemu Mombasani. Majina tajika huku mengi ni ya majazi na wengi wao wamelala korokoroni mara kadhaa. Wale ambao wamevalia mikufu na nyororo aina mbalimbali ndio magwiji wa kutamanika. Wanatembea kama mabingwa wa muziki kule Marekani na kujidai kama wanandondi. Vijana wengi hapa ni maadui wa walinda usalama.

Kakake Magongo ni Mtwapa. Huku ni nyumbani kwa waraibu wa mnazi na tembo aina nyingi. Uchumi wa huku ni wa masaa ishirini na nne. Hili limewezeshwa na uwepo wa vyumba vya kujivinjari vingi hadi vinakaribia kushinda maduka ya kawaida. 

Aidha, 'wauza miili' wanapatikana hapa kwa bei ya mwananchi wa kawaida. Mtwapa ni pahala pema sana kwa wafanyabiashara kwa sababu wateja wapo kila saa hata usiku wa manane.

#MyLifestyle