Mbunge wa akina mama katika kaunti ya Kwale Zuleikha Juma Hassan amekashifu matamshi ya viongozi wanaojifanya wako ODM ilhali wanaongooza wengine katika kutusi viongozi na kuwaambia kuwa hawana maana yoyote.
Akiguzia kufurushwa kwa wabunge Aisha Jumwa (Malindi) na Suleiman Dori (Msambweni) kutoka katika chama cha ODM kufuatia uhusiano wao na Naibu wa Rais William Ruto, Zuleikha alisema "muungano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga haimaanishi kuwa ODM imejiunga na jubilee."
Aliongezea kuwa "kila chama kina sheria zake na kwa wabunge Suleiman Dori na Aisha Jumwa ni kwa sababu wanaunga mkono mgombea wa urais wa chama kingine. Kila chama kinaundwa ili kuingia katika mamlaka. Kwa hivyo ikiwa wewe uko chama kimoja unataka kiingie katika mamlaka inakuwaje wewe unaunga mkono mgombea wa urais wa chama kingine?"
Related: Mishi Mboko warns Aisha Jumwa, Dori days after expulsion
Alisema haiwezikani ila ni kinyume na sheria za vyama vya siasa vya Kenya, akiongezea kuwa vile kamati ya ODM ilivyoamuwa kuwahusu Jumwa na Dori, ni sawa.
"Na vile wanavyosema kuhusu Ruto ni propaganda chama cha ODM hakijatoa rasmi mgombea wa urais atakuwa nani. Nimesisitiza kuwa ni haki ya ODM kuwa na mgombea wa urais, ni sawa pia kwa Raila kusema hatuungi mkono Ruto kwa kuwa hayuko kwa chama chetu."
Akiwahutubia wanahabari siku ya Jumanne, mbunge huyo alisema kupeana mkono na Uhuru haina maana kuwa chama cha ODM kimevunjwa.
"Pengine Ruto akija ODM huenda tukafikiria lakini ODM ina haki ya kuwa na mgombea wao wa urais na jubilee ichague wanaotaka."
#hivisasaoriginal