Rais Uhuru Kenyatta ameungana na wanariadha nchini na nje ya nchi kuombeleza kifo cha bingwa wa mwaka wa 2015 katika mbio za mita 400 kuruka viunzi Nicholas Kiplagat Bett.
Mzaliwa wa Januari 27, 1990, Bett alifariki Jumatano, Agosti 8, katika ajali ya barabarani huko Lessos, kaunti ya Nandi, bonde la ufa.
Mwanariadha huyo alikutana na mauti alipokuwa akielekea nyumbani kwake baada ya kuwasili kutoka kwa mashindano ya ''2018 African Championships in Athletics'' yaliyoandaliwa huko Nigeria.
"Naungana na wanariadha katika kumuomboleza Nicholas Bett ambaye ni bingwa wa mwaka wa 2015 katika mbio za mita 400 kuruka viunzi, na ambaye amefariki kutokana na ajali ya barabarani huko Lessos. Mwenyezi Mungu aifariji familia, ndugu na marafiki wa shujaa huyu," alisema Kenyatta, kupitia kwa mkuu wa mawasiliano kwenye Ikulu, Kanze Dena, muda mfupi baada ya kifo chake Bett.
Pacha wake Bett, Haron Koech, pia ni mwanariadha wa mita 400.
#hivisasaoriginal