Kocha mkuu wa timu ya taifa, Harambee stars, mfaransa Sebastian Migne hatimaye aliweza kusafiri Jumamosi kuelekea Ethiopia na wachezaji watano, miongoni mwao wakiwemo; kipa wa Bandari, Farouk Shikalo na mwenzake Abdallah Hassan, wachezaji wawili wa Gor Mahia, Philemon Otieno na Francis Kahata, na straika wa Kakamega Homeboyz, Allan Wanga.
Kikosi kilichobaki kikijumuisha wachezaji wa kulipwa kinatarajiwa leo alasiri, Addis Ababa kabla ya kuelekea ugani katika jiji la kuu la Bahir Dar.
Migne ambapo awali, alitishia kung'atuka iwapo serikali haitalipa deni lake kabla ya Oktoba 15, analenga ushindi ugenini ili kupongoza shinikizo kwa vijana wanapo jianda kwa mechi ya marudiano Jumapili, dhidi ya Uhabeshi.
"Nitakuwa na muda wa kunoa kikosi, anga siku mbili kabla ya mechi. kwa vile itatulazimu kujituma zaidi ili tupate matokeo bora. Pasi kufanya hivyo tutakuwa na shinikizo kubwa kushinda nyumbani." - alisema Migne
Kutokana na ukosefu wa mapeni kwa mujibu wa shirikisho la michezo nchini, FKF; timu ya taifa haikuwa na kambi ya matayarisho na kwa hivyo kikosi haswa wachezaji wa kulipwa watapata muda mfupi wa kufanya mazoezi pamoja.
Huku hayo yakijiri, Kenya ina nafasi bora ya kufuzu kwenye kipute cha Afcon baada ya kuwa nje miaka 14. Hii ni baada ya Shirikisho la kusimamia soka ulimwenguni, FIFA kuisimamisha kwa muda, shirikisho la soka la Sierra Leone, baada ya serikali kuingilia shughuli za spoti, jambo linalo kinzana na sheria za FIFA.
Marufuku hii dhidi ya Sierra Leone, imeweka hai matumaini ya Stars kufuzu kwa kombe la Afcon, kwa vile imeweza kufutilia mbali ushindi wa Ethiopia wa bao 1 - 0 dhidi ya Sierra Leone na kichapo cha Stars cha 1 - 2 ugenini dhidi ya Sierra Leone.
Ni wamuzi ambawo umeiweka Stars wa pili kwa kundi F na pointi 3 sawa na Ghana, na wanahitaji alama 4 ili kufuzu kwa kipute hicho.
Pia, Uhabeshi na Kenya ndo watakao menyana kwenye mechi ya peke katika kundi hilo, kutokana na marufuku ya muda dhidi ya Sierra Leone.