Picha zifuatazo zinatoa mukhtasari wa maisha ya gavana wa Mombasa, Hassan Johoand.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

 Naibu huyo wa kiongozi wa chama cha ODM hufanya shughuli kadhaa zikiwemo siasa, biashara na kulinda familia. 

Gavana Joho jukwaani na msanii Nyota Ndogo [Picha/nairobiwire.co.ke]

Joho anapenda kujivinjari na kufurahia maisha. Amewaalika wasanii kadhaa Mombasani kujitumbuiza na kuwafurahisha wapwani. Baadhi ya majina makubwa, katika Nyanja ya sanaa Afrika Mashariki, ambayo Joho amealika kufurahisha nafsi yake ni ttanzania Diamond Platinumz na malkia wa pwani Nyota Ndogo.

Biashara

Joho akiwa Marekani kwa shughuli ya kuuza Mombasa Kibiashara [Photo/Kenya-today.com]

Gavana 001 ni tajiri wa kutajika. Ufalme huu wa hela ameutafuta kwa kufanya biashara kadhaa. Zipo picha ambazo zinaonyesha Joho akiwa katika harakati za kujenga biashara yake. Wapo wanaodai kuwa kuna uwezakano kwamba baadhi ya biashara zake haziruhusiwe kisheria Kenya. 

Siasa

Hassan Joho na Rais Uhuru Kenyatta [Picha/Kenya-today.com]

Ukitaja Hassan Joho, wakenya wanamtambua kwa sababu ya harakati zake za kisiasa. Sultani amekuwa naibu wa gwiji wa siasa na waziri mkuu mstaafu Raila Odinga kwa muda. Aidha, amekuwa mpinzani mkuu wa Rais Uhuru Kenyatta pia. Joho alimsaidia sana Bwana Odinga kupata kura Pwani na pia makaribisho yake magharibu yaliwashangaza wengi. Umaarufu wake umemfanya awe kati ya wale watakaokuwa na usemi wa ni nani atanyakua urais mwaka wa 2022.

Familia

Naibu mwenyekiti wa ODM Hassan Joho na watoto wake [Picha/howtodiys.com]

Bwana Joho anaenzi familia yake. Ameilinda na kuiweka kando na siasa na biashara zake. Hii ndio sababu kuu wengi hawatambui bibi na watoto wake.

#MyLifestyle

#hivisasaoriginal