Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amejipata matatani baada ya baadhi ya wanasiasa na wabunge kutoka eneo la pwani kumkemea na kumkosoa kufuatia azimio lake la kutaka urais ifikapo mwaka wa 2022.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongozwa na mbunge wa Msambweni Suleiman Dori, wabunge hao walioasi chama cha ODM ambacho Joho ni naibu kiongozi, wabunge hao walimuonya Joho wakisema yapaswa ajuwe yeye siyo kiongozi wa siasa za pwani.

Walisema Joho anajipendekeza kwao na kwa watu wa pwani, huku akijiita kichwa chao ilihali hatambuliki kama kiongozi wa pwani machoni pao.

Dori alichaguliwa kupitia ODM na kisha kumuasi mkuu wa chama Raila Odinga na kumfuata naibu wa rais William Ruto, ambaye pia yuataka kuwa rais.

Mbunge huyo pamoja na wengine kama Khatib Mwashetani (Lunga Lunga), Kassim Tandaza, Badi Twalib (Jomvu) na Aisha Jumwa (Malindi) walitangaza kuwa watamuunga mkono Ruto, ishara kuwa Joho ana kibarua kigumu mbele yake.

Wanasiasa hao wamekuwa wakizunguka maeneo kama kaunti za Kilifi, Mombasa na Tana River wiki iliyopita wakimpigia debe Ruto huku wakimsuta Joho.

"Hatuwezi kukuskiza kila siku kanakwamba wewe ndiye huelewa kila kitu. Ni lazima utuskize pia sababu sisi ni viongozi ambao twawezafanya chochote ambacho wawezafanya wewe. Hatuweziketi chini na kumskiza mtu ambaye anataka kila kitu kifanyike jinsi atakavyo," Dori ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya wabunge wa pwani (Coast Parliamentary Group - CPG), alisema Ijumaa.

Wabunge hao watakuwa Kombani, Kwale hii leo (Jumamosi) ambapo watakabishwa na mbunge Tandaza.