Miraa hutumika kama dawa ya kupunguza makali ya mawazo mengi, uchovu na kutibu vidonda vya tumbo. Vile vile, miraa ni dawa ya kulevya ya kujichangamsha ambayo inaenziwa Mombasa. Matawi yake hutafunwa na kusababisha uraibu na shida za kisaikolojia. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Yafuatayo ni madhara ya kula miraa kwa wingi:

Ugonjwa wa moyo

Ugonjwa wa moyo waweza kubisha kwa mla miraa kwa uraisi kuliko wale ambao hawali hii chemichemi ya magonjwa. Ikiwa bwanako ataendelea na uraibu huu, kuwa tayari kuitwa mjane.

Kuishiwa nguvu

Mume bila nguvu ni kama mzoga nyumbani. Unyonge wake utavunja nyumba yenu baada ya subira kuisha. Asipoasi miraa, waweza kujaribiwa na pepo la kukosa uaminifu.

Ukosefu wa usingizi

Hatari nyingine ya miraa ni ukosefu wa usingizi. Mumeo atakosa usingizi na hili litaathiri afya yake. Atakonda hata ale vyakula aina gani.

Upungufu wa nguvu za kiume

Hii ndio hatari kubwa sana. Shida zote zinazoletwa na miraa humfanya mwanamume apunguze makali yake wakati wa kujamiana na baadaye kifo kinaweza kufuata ikiwa hatabadili mienendo. Wapo ambao hupoteza hisia za kingono.

Kuna visa vingine ambapo watumiaji wa miraa huvuja damu akilini na ongezeko la hofu. 

Aidha, kina mama ambao wananyonyesha wanao pia wanastahili kuwacha kutumia dawa hii ya kulevya.

#MyLifestyle