Uaminifu ni jambo zuri sana ndoani. Dhamana ya kumuamini mwenzako inafanya kujua ishara za utapeli nyumbani muhimu kwako.
Ikiwa utakuwa na mke mkarimu kugawa ‘mali yako’ kwa kila aombaye, utadhulumiwa kimwili, kifedha na kimawazo. Ingawa wanaume pia huchovia nje, wao ndio huumia sana wakitambua kuwa shamba lao linalimwa na watu wengine.
Ishara hizi zinaonyesha kuwa binti unayefuata ana hulka za kikahaba:
Kujionyesha kupita kiasi
Mwanamke ambaye anang’ang’ana kutambulika kila mahali ni moto wa kuotea mbali. Huyu dada atataka umpe muda wote na siku utakosa kufanya hivyo ataangalia mwanamume mbadala wa kutuliza hamu yake ya kutamaniwa kila saa. Atakuwa tayari kuogelea na yeyote atakayesifu urembo wake.
Marafiki wenye tamaa nyingi za kimwili
Mara nyingi mtu huwa na tabia inayofanana na chenye marafiki wake wanaona chema. Ikiwa kila rafiki wa mchumbao haaminiki, usimuamini pia. Kando na ukweli kuwa kila mtu ana akili za kufanya uamuzi wa kibinafsi, vikundi ambavyo mtu huwa ndani vinaelekeza uamuzi wakati mwingi.
Kutumiana ngono kudhibitisha uke wake
Uke ni zawadi kutoka kwa Maulana na si lazima utumie ngono kuonyesha kiwango cha uke wako. Ikiwa mwanamke anaamini kuwa kulala na wanaume wengi ndicho kigezo cha kuonyesha mwanamke aliye ndani yake, achana naye. Hata umupeleke fungata Marekani, ataendelea kutafuta wanaume wengine ili aonyesha uwezo wake wa kike.
Mpenda hela
Kila binadamu anapenda pesa lakini kiini cha kupenda ndicho kinatutofautisha. Ikiwa mke alikufuata kwa sababu ya hela, hakikisha una hela. Siku utakosa, utaachwa.
#MyLifestyle