Polisi Likoni waliwanasa vijana 14 waliokuwa na mapanga na silaha zingine hatari.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akidhibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba alisema vijana hao ni kati ya umri wa miaka 15 hadi 25.

“Ni vijana wadogo sana na wamekuwa wakiwasumbua wananchi wengi hasa usiku,'' alisema.

Alidokeza kuwa 14 hao walinaswa kwenye upekuzi wa maafisa wa polisi kwenye kivuko cha Feri, operesheni iliyohusisha ukaguzi wa kila mmojai na kufanikiwa kunasa mapanga 13, misokoto 12 ya bangi pamoja na bunduki moja bandia kutoka kwa vijana hao.

'“Tuliwanasa katika kivuko cha Feri wakijaribu kuvuka wakiwa na lengo la kutekelezea uahalifu,'' alisema Simba, Jumatatu.

Kati ya vijana hao, Simba alidokeza kuwa kuwa maafisa wake waliwatambua wanne katiyao, kuwa ni wanachama wa kundi haramu la Watalia.

''Watawasilishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka,'' aliongezea.