Oparesheni hiyo ilifanyika maeneo ya Wild Waters, Mamba village, Nyali City Mall miongoni mwa maeneo mengine ya burudani. /NMG
Watu 20 wamekamatwa kufuatia oparesheni inayoendelea ya kukamata wavutaji wa Shisha mjini Mombasa.
Mkuu wa polisi kaunti ya Mombasa Christopher Rotich alisema kuwa maafisa wa polisi waliwakamata washukiwa hao siku ya Jumanne wakati wa oparesheni maeneo ya Nyali.
Oparesheni hiyo ilifanyika maeneo ya Wild Waters, Mamba village, Nyali City Mall miongoni mwa maeneo mengine ya burudani.
Washukiwa hao watashtakiwa kwa uvutaji wa Shisha ambayo ilipigwa marufuku na serikali tarehe 28 mwezi Disemba mwaka jana.
Katika notisi, Waziri wa afya Cleopa Mailu alisema kuwa uvutaji wa shisha ni hatari kwa afya ya binadamu na kupiga marufuku ya kuagiza Shisha na pia kuitangaza.
“Tumeanzisha oparesheni ya wavutaji wa Shisha na yeyote atakayepatikana atachukuliwa hatua za kisheria,’’ alisema Rotich.
Siku ya Jumamosi waziri wa Utalii Najib Balala aliilaumu serikali kwa kupiga marufuku uvutaji wa Shisha akisema kuwa wengi walikuwa wakitegemea biashara hiyo kama kitega uchumi kwao.
Mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa alisema kuwa maeneo yote yanayotumiwa kwa uvutaji wa Shisha lazima yafungwe