Mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba akiwahutubia wanahabari hapo awali. Picha/ the-star.co.ke
Maafisa wa polisi eneo la Likoni wanawazuilia watu 23 kufuatia msako mkali uliofanywa katika madanguro usiku wa kuamkia leo (Jumatatu).
Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba alisema kuwa watu 10 kati ya walionaswa ni wanawake.Simba alisema kuwa wameanzisha oparesheni dhidi ya biashara haramu ya ukahaba, inayohusishwa na uuzaji wa dawa za kulevya.Alisema kuwa ukahaba umekithirithi eneo la Likoni, huku mahakaba hao wakiendeleza biashara hiyo hata nyakati za mchana.Mkuu huyo wa polisi alisema hali hiyo ni ya kusikitisha kwani baadhi ya waliokamatwa ni watoto wadogo wa shule, walioacha masomo na kujitosa katika biashara hiyo haramu.Wakati huo huo, Simba alisema kuwa polisi wanawasaka washukiwa sita wa ujambazi walioripotiwa kutekeleza wizi katika eneo la Mrima.Washukiwa hao, ambao walikuwa wamejihami kwa visu na mapanga, wanadaiwa kuwavamia wakaazi Jumapili usiku, na kuwahangaisha kwa takriban masaa mawili.Simba aliwahakikishia wakaazi kwamba uchunguzi umeanzishwa na kuahidi kufanya juu chini kuwakamata majambazi hao na kuwachukulia hatua kali za kisheria.