Mwanamume mmoja alifikishwa mbele ya Mahakama ya Nakuru siku ya Jumatano kwa shtaka la wizi wa mabavu.
Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa mshtakiwa, Richard Kimweno, anadaiwa kumshambulia Agnes Wanjiru na kumnyang’anya Sh10,000 miogoni mwa bidhaa zingine, tarehe Septemba 21, 2015 mjini Njoro.
Aidha, upande huo wa mashtaka ulidai kwamba mshtakiwa alitekeleza wizi huo akiwa amejihami kwa silaha butu.
Kimweno alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkuu wa Nakuru Liz Gicheha, aliyemwachilia kwa bondi ya Sh500,000 au 300,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa Novemba 12, 2015, na kusikizwa Disemba 21, 2015.