Wakulima katika kaunti ndogo ya Kangundo katika kaunti ya Machakos wamehimizwa kupanda mimea japokuwa mvua iliyokuwa imetarajiwa imechelewa.
Akizungumza siku ya Jumatano katika ofisi yake, afisa wa kilimo kwenye kaunti ndogo ya Kangundo, Benson Kariuki, alisema kuwa wakulima wengi katika eneo hilo wamekufa moyo baada ya mvua kuchelewa na hivyo kususia kupanda mbegu zao.
"Wakulima wengi katika eneo hili wamekufa moyo kwa sababu mvua imechelewa na nawaomba wasife moyo na waendelee kupanda mbegu zao kwani mvua ipo njiani,” alisema Kariuki.
Vilevile, afisa huyo aliwaomba watu wanaoishi katika maeneo yenye miteremko na ambayo yanaweza athiriwa na mvua kubwa kupanda miti ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.
"Nawahimiza watu wanaoishi maeneo yenye miteremko kupanda miti kuzuia mmomonyoko wa udongo. Nawaomba wasipuuzie tahadhari zinazotolewa kwani wanaweza baadaye,” alisema Kariuki.