Wanabiashara katika kaunti ya Kisii na viunga vyake wameombwa kushirikiana ili kuinua viwango vya uchumi na maendeleo katika eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea siku ya Jumatatu katika uwanja wa Gusii wakati wa uziduzi wa Bendera ya kaunti  mwenyekiti wa chamber of commerce  Benjamin Onkoba amewaomba wanabiashara wote kuungana ili kuendeleza biashara zao kwa njia nzuri.

Onkoba aliwaonya wanabiashara ambao wanatumiwa na baadhi ya watu ambao wana nia ya kusambaratisha maendeleo wakisema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanataka kuharibu biashara zao. 

Aidha, aliwashauri wanabiashara kuwa maandamano sio njia nzuri ya kusuluhisha shida wanazozipitia. 

“Ofisi yangu iwazi. Mazungumzo ndiyo njia bora kusuluhisha shida mnazozipitia kama wana biashara,” alisema Onkoba.  

Onkoba alikashifu wanabiashara walioandamana katikati mwa mji wa kisii mwezi uliopita wakilalamikia kuongezwa kwa kiwango cha ushuru. 

Kwingineko Onkoba aliwaomba wanabiashara hao kuchukulia swala la usalama kuwa la muhimu.

Aliwaomba wanabishara wawe na ujirani mwema.