Wito umetolewa kwa vyuo vikuu kushirikiana na mashirika kutatua changamoto ya malazi unaofikia upeo wa mgogoro.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mtaalam wa uchumi Bi Scholastica Odhiambo wa Chuo cha Maseno ametoa wito kwa wadau wa vyuo vinavyokadhibiwa na mgogoro wa malazi kushirikiana na mashirika kama vile hazina ya hifadhi ya jamii (NSSF) na shirika la ujenzi nchini (NHC) kurobesha miundomsingi

Alisema idadi ya wanafunzi katika vyuo inazidi kuongzeka ilhali miundomsingi haibadiliki. Hali hii alisema inazua changamoto mkubwa kwa vyuo na wanafunzi

Anadokeza kwamba katika shirikiano hizo taasisi zitie sahihi mkataba na wawekezaji. Katika mkataba, alisema, taasisi husika zinatakiwa kutoa mashamba kwa mradi. Baada ya kumalizika kwa ujenzi malazi ikodishiwe wanafunzi na kodi itakayokusanywa kutumika katika kulipa mwekezaji

“Malazi ni changamoto kubwa sana kwa vyuo haswa katika maeneo yasiyoimarika kimiundomsingi. Uhaba wa kifedha unaotokana na mapato ya chini ya wakaazi wa maeneo hayo unasitisha uwekezaji wa kibinafsi; lakini ushirikiano na wadau mbalimbali unawezesha utatuzi wa kudumu,” Bi Odhiambo alisema katika mahojiano.

Mtaalam huyo anasema kwamba shirikiano aina hizo zimezaa matunda kwengineko. Mfumo kama huo ulipitishwa nchini Tanganyika na Chuo kikuu cha Dar es Salaam, alisema.

Aidha aliongeza kwamba idadi ya wanafunzi wanafuzu kujiunga na taasisi za elimu ya juu inaongeka na hivyo kushinikiza taasisi hizo kuweka miundomsingi katika muda mfupi mno

Idadi hii aidha imefanya kupandishwa daraja kwa taasisi za wastani hadi hizo za ngazi ya juu kwa muda mfupi. Hali hii inazorotesha zaidi mgogoro wa miundomsingi

“Ingawaje mfumo mpya wa elimu unaboresha ujuzi na utendakazi , hali mbaya ya taasisi inadhuru wanafunzi,” alisema.

Chuo Kikuu cha Kenyatta ambacho ndicho kubwa zaidi nchini kwa idadi imesifiwa kwa juhudi za kuboresha malazi ya wanafunzi.

Februari mwaka jana chuo hicho kilizindua mradi wa malazi kwa wanafunzi 6, 000.

Hii ilikuwa mradi wa kwanza wa aina hiyo nchini. Chuo kilitoa shamba ekari 20 kwa madhumini hayo. Asilimia 54 ya wanafunzi katika chuo hicho wanishi katika malazi yaliyojengwa na shule.

Wanafunzi 123, 000 walifuzu kujiunga na taasisi za elimu ya juu katika mtihani wa KCSE mwaka jana.