Wazazi wa shule ya msingi ya Matutu wadi ya Gesima eneo bunge la Kitutu Masaba, wamempongeza mwanasiasa Mokaya Maroko kwa kuipatia shule hiyo gunia za mahindi.
Wakiongea katika shule hiyo hapo jana wakati wa kupokezwa zawadi hiyo wazazi hao walimpomngeza mwanasiasa huyo na kusema hiyo ni njia moja ya kuinua viwango vya masoma katika wadi ya Gesima .
“Tuko na shukrani kwa mheshimiwa Mokaya Maroko kwa kukumbuka shule yetu ya Matutu kwa kutupatia msaada wa mahindi ili wanafunzi wapate chakula na kuendelea na masomo yao,” alisema Salome Kenyoni mkaazi.
Aidha, wazazi hao wamewaomba viongozi wengine kuiga mfano huo na kufadhili miradi mbalimbali ili kuinua viwango vya mandeleo hasa katika sekta ya elimu.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Patrick Nyangeri alipongeza hatua hiyo iliyochukuliwa na Mokaya Maroko na kusema kuwa mahindi hayo yatasaidia pakubwa katika muhula wa pili kwa kuwa wanafunzi watakuwa na chakula cha kutosha ikilinganishwa na nyakati zilizopita.
Nyangeri, alisema kuwa wakati wanafunzi huendea katika chakula cha mchana, wengi wao hurudi shuleni wakiwa na njaa kwani huenda wanakosa chakula.
Mwalimu huyo mkuu ameomba wafadhili wengine kujitolea na kuisaidia shule za msingi na misaada mbalimbali ili kuinua viwango vya masomo .
Kwa upande wake mwanasiasa Mokaya Maroko alikiri kuwa yeye yuko tayari kushirikiana na wazazi wote wa shule mbalimbali katika wadi hiyo ya Gesima ili kuinua viwango vya masomo .
“Niko tayari kushirikiana na wazazi wote ili kuinua viwango vya masoma na kuwapa wanafunzi motisha ya kufanya bidii masomoni.