Visa vya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana katika kaunti ya Nyamira vinazidi kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Haya ni kulingana na mkurugenzi wa kisaikologia kwenye wizara ya mahusiano ya Africa mashariki Agnes Sila.

Sila alisema kuwa viwango vya ukosefu wa ajira kwa vijana vinaendelea kuongezeka hata zaidi, huku Nyamira ikiwa imeadhirika pakubwa

Akizungumza kwenye mkutano wa washikadau uliopangwa na serikali ya kaunti ya Nyamira siku ya Jumanne, Sila alisema kuwa yafaa serikali ya kitaifa na ile ya kaunti zishirikiane kuhakikisha kuwa changamoto zinazowakumba vijana zinatatuliwa kwa haraka ili kuwawezesha vijana kujiendeleza.

“Serikali ya kitaifa na zile za kaunti zinafaa kuhakikisha kuwa shida na matatizo wanayopitia vijan, haswa ukosefu wa ajira yanatatuliwa ili vijana waweze kujiendeleza,” alisema Sila.

Afisa huyo aliongeza kwa kusema kuwa swala la ukosefu wa ajira husababisha vijana kujiunga na makundi ya uhalifu, hali inayodhalilisha uchumi wa taifa hili.

“Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana husababisha wengi wao kujiunga na makundi ya uhalifu, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa yanaathiri uchumu wa nchi,” aliongezea.

Mkutano huo uliwaleta pamoja waziri wa masuala ya jinsia na vijana Peter Omwansa na wakurugenzi mbalimbali ya masuala ya vijana.