Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imemkamata mhandisi mmoja wa kampuni ya kusambaza nguvu za umeme nchini KPLC tawi la Ukunda kwa tuhuma za ufisadi.

Kulingana na mkurugenzi wa tume hiyo eneo la Pwani Hassan Khalid, mhandisi huyo alipokea hongo ya shilingi elfu 15 pesa taslimu kutoka kwa mkaazi wa eneo la Diani -Ukunda akidai kumuwekea nyaya na nguvu za umeme kwa njia ya mkato.

Akiongea na wanahabari baada ya kumtia nguvuni mshukiwa huyo na kumhoji Jumatatu mjini Mombasa, Khalid alisema kwamba visa vya maafisa wa idara mbalimbali na viongozi kuitisha hongo kwa wakazi na wafanyibiashara ili kuwasaidia vimekithiri na akasema kwamba lazima kwa hatua kali dhidi ya watu kama hao kuchukuliwa.

“Tumemkamata mhandisi huyo akipokea hongo shilingi elfu 15 pesa taslimu kwa mkaazi wa eneo la Diani – Ukunda akidai kuwa atamuwekea nyaya na nguvu za umme kwa njia ya mkato. Hiyo tumekuwa tukiwafatilia kwa ukaribu sana watu kama hao na sasa tumewakamata.Wako watu wengi sana wanaitisha pesa kwa wakazi ndio wawezekuwasaidia tutawakamata na kufungulia mashtaka,”alisema Khalid.

Khalid amewahimiza wakazi kushirikiana na maafisa wa tume hiyo kwa kutoa habari kuhusu maafisa wa idara mbalimbali na viongozi pamoja na wakazi wanaoshiriki ufisadi kuchunguzwa na kutiwa nguvuni ili kufunguliwa mashtaka.

“Tunawaomba wakazi kushirikiana na maafisa wetu kwa ukaribu sana na kutusaidia na bahari kuhusu watu kama hawa naopenda kuitisha pesa ili tuwachunguze na kuwakamate kisha tuwafungulie mashtaka mara moja,” aliongeza Khalid.

Mshukiwa huo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Bandari akisubiri kukamilika kwa uchunguzi kabla ya kufikishwa mahakamani hii leo.