Wahudu wa Matatu wametaka Maafisa wa Trafiki mjini Kisumu kuboresha uelekezaji wa magari kwenye barabara za mji ambazo zimeanza kuwa na msongamano mwingi nyakati za asubuhi na jioni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wahudumu hao ambao walipasha hoja hizo kupitia kwa Mwandishi huyu, walisema kuwa barabara zinazokarabatiwa kwenye mzunguko ulioko katika mlango wa kuingia uwanja wa Kenyatta Sports Ground zinahitaji uelekezi wa Afisa wa Trafiki ikizingatiwa kuwa ndio mzunguko unaounganisha magari yanayoingia na kutoka jijini pamoja na yale ya huduma za mji.

“Mzunguko huu unatukalisha sana barabarani kwa kuwa wakati mwingi huwa hatuelekezwi na Afisa yeyote wa Trafiki na hivyo basi kila dereva anajitafutia namna anavyo weza kupenya na kuharakisha safari yake bila kuwajali wengine kwenye barabara hilo amblo pia hua kwa haraka,” alisema Bobby Juma dereva wa Matatu ya huduma wa mji, almaarufu Town Service.

Barabara ya Jaramogi Oginga Ondinda ambalo pia linaelekea kwenye mzunguko huo, hua na msongamano na foleni ndefu ya magari ambayo husonga kwa mwendo wa kinyonga haswa saa za jioni na wakati mji huo unapokua na shughuli kama vile za kisiasa na kitaifa.

Aidha wahudumu hao walitaka ukarabati pamoja na ujenzi wa barabara nyinginezo mpya zinazoendelea kujengwa jijini humo kuharakishwa ili kuwapa nafuu wanapokuwa barabarani.

Pia wahudumu hao waliwaomba wenzao wa Bodaboda ambao pia ni wahudumu kwenye barabara hizo za mji kuonyesha heshima kwa wenzao wakiwa barabarani, kwa kujali masilahi na maisha ya wateja wao ambao huwa mikononi mwao wakati huo wa kazi.