Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi wilayani Kenyenye eneo bunge la Bomachoge Borabu, wana kila sababu ya kutabasamu baada ya ofisi ya kupeana vyeti vya kuzaliwa na vile vya kifo kufunguliwa.

Hii ni baada ya wakazi hao kulalamika kuwa wao hulazimika kutembea muda mrefu hadi eneo la Ogembo ambapo ofisi hiyo inapatikana.

Ofisi hiyo ilifunguliwa siku ya Alhamisi kando na ofisi ya eneo bunge la Bomachoge Borabu.

Wakazi wa eneo hilo walipongeza usimamizi wa eneo bunge hilo kwa kuitikia wito wao na kilio chao kwa kushughulika haraka iwezekanavyo.

Ofisi hiyo itaanza kutumika rasmi siku ya Jumatau juma lijalo.

“Tumekuwa tunasumbuka kutembea safari ndefu kutoka eneo hili letu wilayani Kenyenya hadi eneo la Ogembo kufuatilia vyeti vya kuzaliwa vya watoto wetu ambavyo huhitajika wakati wanajisajili katika mtihani wa kitaifa. Uvumbuzi wa ofisi hiyo umetuletea furaha tele,” alisema Jackson Omariba, mkazi wa eneo hilo.

“Mimi napongeza usimamizi wa eneo bunge letu hasa mbunge Joel Onyancha kwa kutufungulia ofisi hii katika wilaya ya Kenyenya. Hayo ndio maendeleo yanayotusaidia sisi kama Wakenya wa kawaida,” alisema Cecilia Nyakundi, mkazi.