Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bweni ya wanafunzi 131 katika shule ya wavulana ya Moi Gesusu iliyoko eneo bunge la Nyaribari Masaba kaunti ya kisii iliteketea usiku wa kuamkia leo na kusababisha hasara ya mali isiojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo siku ya Jumanne katika shule hiyo, mwalimu mkuu Naftal Ochora alisema bweni hilo lilichomeka mwendo wa nane usiku, huku chanzo cha moto huo kikiwa hakichabainika hadi sasa.

Kulingana naye, hii ni mara ya kwanza shule hiyo kuchomeka kupitia mkasa wa moto, huku mkasa huo ukiwaacha wengi vinywa wasi haswa wakazi na wananchi wote kwa ujumla

“Wanafunzi ambao tuko nao shuleni kwa sasa ni wa kidato cha nne ambo wanaendelea kudurusu na kujitayarisha kwa mtihani wa kitaifa na ni hao sasa wameathirika pakubwa kupitia mkasa huu wa moto,”alisema Ochora.

Afisa wa elimu katika kaunti ya Kisii David Kebiro alifika shuleni humo huku akisema uchungunzi uanzishwe mara moja ili kubaini chanzo cha mkasa huo kwani shule nyingi zimekuwa zikichomeka kila mara.

Wakati huo huo, afisa anayesimamia mikasa katika kaunti ya Kisii Patrick Lumumba alishangazwa na mkasa huo, huku akiomba uchungunzi kuharakishwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliomba wahisani wema kujitolea kutoa usaidizi kwa wanafunzi hao 131 ambao walipoteza vitabu, malazi, sare za shule na vinginevyo