Kilikua kioja mjini Naivasha siku ya Alhamisi wakati matapeli wawili wa kike waliponaswa mjini humo wakitaka kumtapeli mwanamke mmoja jumla ya shilingi elfu kumi na tano.
Inasemekana kwamba wanawake hao walimwandama mwamke huyo hadi kwenya benki ya Kenya Commercial Bank tawi la Naivasha, ambapo walimdanganya kuwa wanaweza mwombea ili pesa hizo ziongezeke.
Mwanamke huyo, kwa jina Gladys Wanjiru, alisema wezi hao walokua tayari wamenyakua pesa zake baada ya kumdanganya, lakini baadaye akagundua kua alikua ametapeliwa.
Wanjiru aliweza kupiga kamsa iliyovutia umati mkubwa ambao ulitaka kuwateketeza wanawake hao wawili.
"Nilikua tayari nimewapa pesa lakini nikagundua kwamba nilikua nimetapeliwa, hapo ndipo nilipopiga kamsa na umati wa watu ukaja na kukamata matapeli hao," asema Wanjiru.
Polisi waliokua wakipiga doria waliweza kuwaokoa matapeli hao kutoka kwa mikono ya wananchi, na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Naivasha.
Naibu mkuu wa polisi mjini humo Jane Ajamong alidhibitisha kisa hicho na kutaadharisha wananchi dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao.