Wakazi wa eneo la Riosiri, wilaya ya kenyenya kaunti ya Kisii wameiomba sekta ya afya na wahisani wema kuwatembelea na kuwapea tiba ya funza.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongea katika hospitali ya Rufaa na mafunzo ya Kisii siku ya Jumamosi mchana, Nyanya na mamake mtoto mmoja wa miaka mitatu aliyeletwa baada ya kuvamiwa na funza, nyanya huyo aliwaomba wahisani wema kutembelea hadi nyumbani  kwake ili kumsaidia kukabiliana na funza hao.

“Naiomba serikali ya kaunti ya Kisii kupitia sekta ya afya kutembelea kijiji chetu kwa kuwa funza wametusambua ili watusaidie na dawa,” alihoji nyanya.

Jane na mamake  shalon Kemunto ambaye alikuwa ameathiliwa na funza  katika nyayo zake hata kutembea kwake kulikuwa na shida kubwa walimuleta hasdi hospitalini ili kupewa dawa.

Kwingineko, akiongea wakati wa kumtibu mtoto huyo, Kepha King’oina ambaye ni mhudumu wa afya ya Jamii katika kaunti ya Kisii alisema kuwa kutokana na umaskini mwingi na kupuuza mawaidha wanaotoa kwa Jamii ndio chanzo cha funza hao.

Kwa sasa amewaomba jamii na jamaa zao kuwajibika na kuboma nyumba zao na kuhakikisha kuwa mahali wanamoishi ni pasafi, ili kujikinga kutoka  kwa funza hao ambao wanawaathiri watoto wadogo ambao wanastahili kuwa shuleni.

“Umaskini na kupuuza mawaidha yanayotolewa kwa jamii nyingi ndio sababu kuu ya Jamii kushambuliwa na funza hawa, ni heri kila mtu awajibike na kujua kuwa afya ni kitu cha mhimu sana, na ni bora kinga kuliko dawa,” alihoji King’oina.

Aidha, King’oina amewaomba wasimamizi wa afya kutoka kaunti ya Kisii kuchukulia swala la funza kuwa janga kubwa linalowasumbua watu wengi katika jamii na kuchukua msaada wao ili kuwasaidia wananchi.