Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mfanyikazi mmoja katika benki ya Diamond Trust amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la wizi.

Upande wa mashataka ulieleza mahakama kuwa kati ya tarehe Oktoba 2, 2015 na 5, 2015 mshtakiwa, George Nzivu, anadaiwa kuiba dolla 120 ambazo ni sawia na shillingi 13,400 za Kenya, kutumia jina la Sheila Akinyi mteja wa benki hiyo.

Mshtakiwa alikana madai hayo ya wizi mbele ya Hakimu Diana Mochache siku ya Ijumaa.

Hakimu Mochache alimwachilia mshtakiwa huyo kwa kumtoza dhamana ya shilingi 100,000 au shilingi 50,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itasikizwa tena Januari 15, 2015.