Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa Kangundo katika Kaunti ya Machakos Bwana Kyengo Maweu amewataka watahiniwa wa kidato cha nne kujiepusha na kila aina ya udanganyifu kwenye mitihani ya kitaifa.

Akizungumza katika ofisi yake siku ya Jumanne, Bwana Maweu aliwaomba watahiniwa hao kuwa watulivu na kujiamini wanapofanya mtihani na kutokubali mgomo wa walimu uliopita kuwaadhiri kiasi cha kutaka kudanganya katika mtihani.

"Nataka kuchukua fursa hii kuwatakia mema watahiniwa katika eneo la Kangundo na nchi nzima kwa jumla wakati huu ambao mitihani ya kidato cha nne unaendelea,” alisema Bwana Katatha.

Aliongeza, "Ningewaomba sana msiweze kuathiriwa na mgomo wa walimu uliofanyika mkadanganyika na kutaka kujihusisha na udanganyifu katika mtihani."

Mitihani ilianza vyema Katika eneo hilo la Kangundo na kufikia wakati huu, hakuna shida au visa vya udanganyifu vimeweza kuripotiwa.