Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana walioajiriwa katika mradi wa NYS waliandaa maandamano jijini Mombasa Jumatatu kulalamikia hatua ya serikali kutowalipa mishahara yao.

Kulingana na vijana hao, hawajapata kulipwa pesa zao licha ya kuajiriwa miezi mitatu iliyopita.

"Ni jambo la kusikitisha sana kuwa bado hatujalipwa pesa zetu wakati tumefanya kazi kwa zaidi ya miezi miwili sasa," alielezea mmoja wao.

Vijana hao waliajiriwa katika mradi huo miezi mitatu iliyopita bila kupata mshahara wa mwezi mmoja kutoka kwa serikali, na kuwaomba viongozi wa kaunti hiyo kuwajibika ili wapate haki zao.

"Tunamwomba gavana Hassan Joho na mbunge wetu wachukue hatua dhabiti kutatua swala hili kwa haraka iwezekanavyo," alielezea zaidi.

Rais Uhuru Kenyatta mapema mwezi Septemba alizindua mradi wa NYS jijini Mombasa, huku ikiwa na lengo ya kuajiri zaidi ya vijana 1,000 kufanya kazi za kusafisha jiji hilo.