Mke wa Gavana wa Kaunti ya Kilifi Bi Liz Kingi amewakata wakazi kuungana katika kampeni ya kumaliza funza katika jamii.
Kulingana na Bi Liz, wakazi wengi katika vitongoji duni wameathirika na funza na kuna haja ya kuidhinisha mikakati mwafaka ya kuangamiza kuenea kwa funza miongoni wa wakazi.
Akizungumza na wanahabari baada ya kuhudhuria kongamano la hamasa mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Bi Liz alisema kwamba funza wameathiri jamii kwa kiwango kikubwa na kuna haja ya hatua kidhinishwa.
“Tunazishiniza serikali za kaunti kuhakikisha kwamba zinachangia katika kampeni za kuangamiza funza mashinani ili kuona kwamba jamii inaishi bila changamoto za maradhi hayo”,alisema Bi Liz.
Kwa upande wake kiongozi wa wanawake kaunti ya Mombasa Bi Afiya Rama amewashikiza wahisani kujitokeza na kusaidia kufanikisha juhudi za kuangamiza funza kupitia kampeni hiyo.
Aidha amewataka viongozi wa kisiasa kuungana na wadau mbalimbali kufanikisha kampeni ya kumaliza funza katika maeneo ya mashinani ili kuwasaidia wakaazi kujiepuka.