Wakaazi kutoka eneo bunge la Nyaribari chache kaunti ya Kisii wamemshukuru Rais Kenyatta kwa uteuzi aliyofanya kwa Bodi mbalambali na kukumbuka Jamii ya kisii.
Wakaazi hao walikusanyika jana katika boma la aliyekuwa mbunge wa eneo hilo la Nyaribari Chache, dakrari Robert Monda, ilioko kijiji cha Kerera.
Walimshukuru na kumpongeza Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kwa kumchagua Robert Monda kuwa mwenyekiti wa Bodi ya ‘Creditation Service Boad’ of Kenya.
Wakaazi hao walisema uteuzi wa rais ni njia mojawapo ya kuonyesha kuwa anakumbuka Jamii ya wakisii kwa ujumla huku wengi wao wakisema ifikapo mwaka wa 2017 watampigia kura za kumrudisha kwa kiti cha urais.
“Tunasema asante kwa Kenyatta na kukikuwa na nafasi nyingine tunamwomba atukumbuke tena,”alisema Christopher Ondieki, mkaazi.
“Mimi nikona na furaha kwa rais wetu kwa kumchagua aliyekuwa mbunge wetu kuwa mwenyekiti na ninasema wakisii wote tuko na imani kwa rais wetu na 2017 tutamchagua tena,”alisema Nyasuguta Ogega mkaazi.
Kwa upande wake daktari Monda, aliyechaguliwa hakuficha furaha yake kwa kuchaguliwa na kusema rais ni mtu wa kukumbuka Jamii zote zilizoko hapa Kenya.
“Namshukuru Rais Kenyatta kwa kunichagua kuwa mwenyekiti wa Bodi ya ‘Creditation Service Boad’ na ninamahidi kufanya kazi kikamilifu na kwa uwazi kwa wakenya wote na niko na furaha nyingi kwa rais wetu. Namsihi andelee kukumbuka na kufanyia wananchi kazi kwa uwazi jinsi alivyofanya kwa uteuzi na nitafanya kazi na serikali ya Jubilee mpaka mwisho,” alisema Monda.