Katibu mkuu wa Baraza la Maimamu tawi la Mombasa, Sheikh Mohamed Khalifa, amekashifu tukio lililofanyika katika Chuo kikuu cha Strathmore jijini Nairobi, ambalo lilisababisha kifo cha mfanyikazi mmoja, huku wanafunzi 20 wakiachwa na majeraha.
Akizungumza siku ya Jumanne, Khalifa alisema kuwa waliohusika na tukio hilo sharti wakabiliwe kisheria ikizingatiwa walisababisha kifo cha raia bila hatia.
Aidha, alionyesha kusikitishwa na jinsi zoezi hilo lilivyoendeshwa pasi kujulishwa wanafunzi wa chuo hicho ili kujitayarisha vyema.
Jaribio hilo la namna ya kukabiliana na tukio la kigaidi lilifanywa na idara ya polisi.
Milio ya risasi ilisikika chuoni humo iliyowafanya wanafunzi kutaharuki na kuruka kutoka ghorofa walimokuwa wanasoma ili kujiokoa.
Usimamizi wa shule hiyo utasimamaia gharama zote za matibabu za wanafunzi waliojeruhiwa.