Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kijana wa umri wa makamo amefungwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kumtusi mama mkwe wake.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, Hakimu Susan Shitub alisema hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaopenda kutumia matusi kupitia vifaa vya mawasiliano.

Mahakama ilielezwa kuwa mnamo Agosti 24 mwaka huu, katika eneo la Bomani huko Likoni, Hamisi Malibaka anadaiwa kumtusi Mariam Burudani kupitia simu yake ya mkono, matusi yanayodaiwa kutatiza amani.

Malibaka alikubali makosa hayo na kusema kuwa alikuwa na hasira baada ya kukorofishana na mpenziwe.