Wakaaji wa Kisii wamewaomba wenye maduka na nyumba katika mji huo kuchukulia swala la usalama  kwa umuhimu kwa wateja wao na hata kwa wafanyikazi kwani  ni bora kukinga kuliko kutibu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Swala hili linaibuka wiki moja baada ya kamishna wa kaunti ya Kisii Chege Mwangi kuwawakikishia wakaazi wote kuwa kuna usalama wa kutosha, na kuwaomba wenye maduka ya jumla na wengine kuchukulia swala la usalama kuwa muhimu kwao.

Wakiongea Ijumaa asubuhi nje ya duka la jumla la Tuskys, baadhi ya wakazi hao walisema kuwa ukaguzi  katika baadhi ya maduka hayo ya jumla katika mji wa Kisii unafanywa kwa njia ya mzahaa, na ni duni, kitu ambacho wenye maduka hao wameombwa kufanya kwa njia inayostahili na kukagua watu kabla hawajaingia katika duka lolote.

Peter Nkege ni mmoja wa waliosema kuwa maduka hayo sharti yahakikishe kuwa ukaguzi wa kutosha umefanyia kwa wanunuzi kikamilifu, kwa kuwa hiyo ndio njia moja itaweza pkusaidia kuebukana na janga la mashambulizi.

“Walinzi wanaokagua watu wanoingiaa kwa maduka hayo wanastahili kufanyiwa ukaguzi kikamilifu nawalinzi husika na kuweka kando mzaha, ukaguzi huo hata watoto wanastahili kukaguliwa kabla ya kuingia,” alihoji Peter Nkege.

Kwa upande wake, mama Teresia Bosibori alisema kuwa ameshuhudia siku nyingi, hasa wakati anaingia katika baadhi ya maduka anafumania mkaguzi na mmoja ambaye ni mwanaume  kumrusu kupita bila kumkagua kwa kuwa  mwanaume harusiwi kumukagua mwanamke, jambo amesema wenye maduka hayo ya jumla wanastahili kulifanyia marekebisho na kuhakikisha kuwa mwanamke sharti awe kila wakati kwa ukaguzi kamili.

Aidha, wamewaomba wakaazi wengine kuunga mkono na kuendeleza mradi wa serikali wa nyumba kumi, kwa kuwa hilo ni jambo la muhimu sana kwa wakenya wote.

Kwingineko, wenye makanisa katika mji wa kisii nao wameombwa kuweka walinzi na wakaguzi katika milango na kukagua watu kikamilifu kabla ya kuingia dani ya kanisa.