Mwalimu wa shule ya msingi ya Mochenwa anayekabiliwa na tuhuma za uvujaji wa shillingi elfu 250,000, pesa zilizotengewa kufanyia miradi shuleni, sasa anamlaumu mwanasiasa flani kwa kumsababishia shtuma zinazomkumba kuhusiana na uvujaji huo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwalimu huyo, Kefa Nyangaresi, alimshtumu aliyekuwa diwani wa zamani wa eneo hilo kwa kuwachochea wazazi dhidi ya uongozi wake, huku akiongeza kusema kuwa pesa hizo zilitumika kununua vitabu vya kusoma na pia kuwafadhili wanafunzi kutoka idara ya spoti walio wakilisha shule hiyo kwenye mashindano ya mkoa katika chuo kikuu cha Kisii. 

"Kila rekodi ya matumizi ya pesa shuleni humu ni wazi kwa kuwa pesa hizo zilitumika kununua vitabu vya kusoma na pia kuwafadhili wanafunzi wa idara ya michezo walio wakilisha shule hii kwenye mashindano ya mkoa kule chuoni Kisii, ila kazi ya diwani huyu wa zamani ni kuwachochea wazazi dhidi yangu kwa sababu nisizozielew," alisema Nyangaresi. 

Aidha, mwalimu huyo aliiomba wizara ya elimu kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tuhuma hizo na kisha kuwawekea vikwazo wanasiasa kutoingilia maswala ya usimamizi wa shule ili kuwalinda walimu wengine wanaokumbana na tuhuma sawia na zake. 

"Naheshimu sheria, na hii ni siasa tu inayochezwa. Naiomba wizara ya elimu kuingilia kati na kufanya uchunguzi wake wa kina kuhusiana na tuhuma za utumizi mbaya wa afisi na ikewezekana iwawekee vikwazo wanasiasa kutoingilia shughuli za usimamizi wa shule za umma ili walimu wengine walio na changamoto sawia na zangu wakaweze kulindwa na sheria," alisihi Nyagaresi. 

Haya ya najiri baada ya baadhi ya wazazi kufanya maandamano siku ya Jumatatu kulalamikia uongozi wa mwalimu huyo, huku wakitaka tume ya uajiri wa walimu imwachishe kazi.