Wakulima kutoka Jimbo la Nakuru watanufaika zaidi na mpango wa mbegu na mbolea za bure ikilinganishwa na mwaka jana.
Haya ni kwa mujibu wa afisa msimamizi wa kilimo Purity Muritu aliyesema kuwa hii ni kufuatia bajeti ya chini iliyotengewa mpango huu.
Akiongea katika hafla moja mjini Nakuru Muritu amesema kuwa kinyume na mwaka jana ambapo mpango huo ulitengewa Sh15 millioni tu huku mwaka huu ukitengewa Sh60 millioni kwa mpango husika.
Muritu amesema kuwa wamebaini Wadi 48 ambazo matokeo zao huwa safi zaidi akihoji kuwa wakulima 1,000 kutoka kila Wadi hizo watanufaika na mpango huo kinyume na wakulima 75 kutoka kila Wadi mwaka jana.
Aidha, amewataka kutayarisha mashamba yao mapema kwa upanzi wa vyakula vinavyokua haraka akihoji kuwa ni mvua chache inayotarajiwa katika mwezi wa Aprili sawia na Mei.
Kiongozi huyo hata hivyo ameitaka Serikali Kuu kufanya mpango wa kupeana chakula cha msaada kufuatia kuathirika kwa mahindi katika mengi ya maeneo ikiwemo Njoro, Naivasha, Gilgil na hata Subukia.