Mwanaume mmoja alifikishwa katika mahakama moja mjini Nakuru siku ya Jumatatu kwa kosa la kumbaka msichana wa miaka 13.
Mahakama ilielezwa kuwa tarehe Septemba 28, 2015 katika eneo la Coolers, viungani mwa mji wa Nakuru, Austin Barasa anadaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 13.
Upande wa mashtaka aidha ulisema kuwa siku hiyo, mshtakiwa Barasa alimkosea heshima msichana huyo kwa kumgusa kwenye sehemu zake za siri.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Joel Ng’eno na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh70,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itasikizwa Oktoba 15, 2015.