Wahudumu wa magari wanaotumia barabara ya Ram - Prisons wamewalaumu baadhi ya vijana wa bodaboda na wale wa kuosha magari kwa kushirikiana kuziba mabomba ya maji kwenye mto Nyakumisaro.
Wahudumu hao wameilalamikia serikali ya kaunti ya Kisii kwa kukosa kurekebisha na kushughulikia daraja hilo kulingana na ahadi waliyotoa kuwa daraja hilo litatafutiwa suluhu.
Akiongea siku ya Jumatano kwenye steji ya magari ya kutoka Kisii kuenda Nyamira, mwenyekiti wa magari ya Ziwaline Sacco, Joel Osoro Mokaya, alilalamika kuwa daraja hilo limekuwa likifurika kila mara na kuwapa kazi ngumu kuzunguka hadi daraja moja hali ambayo mara nyingi husababisha msongamano mkubwa kwenye barabara ya Kisii Keroka.
Alishangaa ni kwa nini serikali ya kaunti haitafuti suluhu la haraka kwa kurekebisha daraja hilo. Amesema kuchimbua mashimo pana ya kupitisha maji chini ya daraja hilo ni finyu mno na ndio chanzo cha kuleta mafuriko na kufunga barabara.
Alisema kuwa imekuwa sasa ni mtindo kwa wengi wa vijana wa bodaboda kushirikiana na baadhi ya vijana wa kuosha magari kuziba mabomba hayo ya kupitisha maji hasa nyakati za mvua ili maji yajae barabarani nao waweze kuvusha watu kwa ada ya shilingi ishirini.
"Baadhi ya vijana wana mtindo wa kufunga na kuziba karafati za kupitisha maji kwenye mto huo wa Nyakumisaro eti ndio watengeneza hela kupitisha na kuvusha watu kutoka upande mmoja kuenda mwingine ambayo ni kinyume cha sheria.