Wakaazi wa kijiji cha Nyabomite, wilayani Nyamira eneo bunge la Mugirango Magharibi  wameikashfu  serikali ya kaunti hiyo kwa kutotengeneza barabara mbaya katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi hao walikuwa wakiongea na mwandishi huyu siku ya Jumatatu baada ya gari la shirika la usalama la G4s lilianguka na kugonga nyumba ya mkaazi mmoja kwa jina Dolphine Kemunto usiku wa kuamkia leo na kunusurika kifo katika barabara ya kutoka eneo la Gianchore kuelekea Nyamira.

Wakaazi hao walionekana kughadhabishwa na jinsi serikali hiyo haifanyi maendeleo, hasa kuzikarabati barabara ambazo ni mbovu na kuendelea kusababisha ajali katika eneo hilo kila kuchao.

“Uongonzi wa kaunti hii ni mbaya maana viongonzi walio kwa viti hawataki kuzitengeneza barabara mbovu. Unaona mkaazi huyu mwezetu angeuawa usiku wa kuamkia leo wakati gari liligonga nyumba yake na mvua ilikuwa inanyesha, jambo lilisababisha gari hilo kuteleza ni barabara mbaya, twaomba serikali itukumbuke,” alihoji Justine Morara, mwanakijiji wa Nyabomite.

Serikali ya Nyamira, ikiongonzwa naye gavana John Nyagarama pamoja na wawakilishi wa wadi mbalimbali wameombwa kuzikarabati baadhi ya barabara mbaya katika kaunti hiyo ili kupunguza ajali zinazoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo

“Tuliwachagua viongozi ili kubadilisha maisha yetu kwa kuanzisha miradi mbalimbali na kutengeneza barabara mbaya katika eneo hili, lakini ni kama hawataki kutimiza yale walituahidi sasa tuwafanyie nini?” aliuliza Nehemia Ogembo, mkaazi mwingine wa kijiji hicho cha Nyabomite.