Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Chifu mkuu wa kata ya Kiamaina Jones Kariuki Nduati ametahadharisha wenye biashara za video, vilabu na michezo ya pool ambao wanaruhusu watoto wadogo na wanafunzi kuingia kwenye vyumba hivyo kuwa watakamatwa.

Nduati akiongea na mwandishi huyu kwenye ofisi yake iliyo eneo la Kiamaina Maili Sita kaunti ya Nakuru, alisema amepokea malalamishi hayo, ila wanapanga kushirikiana na serikali ya kaunti na ajenti zingine, ili kunyaganya leseni wote watakaokiuka sheria hizo wakati huu wa likizo ya Disemba.

Chifu huyo vile vile aliwataka wazazi kuwa mfano mwema kwa watoto wao, na kukoma kwenda kwenye vyumba vya burudani wakiwa na watoto wachanga, akisema hilo linaharibu kizazi cha kesho.

“Ni aibu kupata habari kwamba hata wanawake walio na watoto wadogo huingia kwenye vyumba hivyo, pasi na kujiuliza kama ataepuka mkasa kama wa stima ukiweza tokea”.

Hivyo aliwataka wanabiashara hao kutii sheria, kabla ya kutiwa mbaroni.

Wazee Joseph Kamau na Gilbert Nyakundi, wote wakaazi wa eneo hilo, walisema msako huo utasaidia pakubwa kupigana na uovu ulio kwenye jamii, kwani sasa dawa za kulevya zinauziwa kwenye video na vyumba vya pool.

“Watoto wamekosa wa kuwashauri, vijana wanavuta sigara na bangi pamoja na wazee. Kheri zifungwe kama wenyewe watashindwa kuzuilia wanaouza dawa na miraa kwenye kazi zao” akasema bwana Kamau.

Naye Nyakundi aikosoa wazazi ambao hutazami filamu na video za mapenzi kwenye runinga wakati ambapo watoto wao hawalala.