Wakristo wote wameombwa kuwa katika mstari wa mbele kwa kuhuburi amani na upendo miongoni mwa wakenya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea hiyo jana katika kanisa mpya la Pentecost assembly of God Nyamakaroto katika wadi ya Gesima eneo bunge la Kitutu Masaba, aliyekuwa mkuu wa kanisa katika wilaya ya Nyansiongo Josheph Mosoti aliwaomba wakristo kuwa wa kwanza kuiombea nchi.

Mosoti aliwaomba wakristo wote kuungana pamoja na kuwa na imani moja ya kuombea nchi, kwa kuwa ndio njia moja ya kumuuliza mungu kuisaidia nchi ya Kenya hasa wakati huu ambapo swala la ndoa ya jinsia moja inaendelea kuibua maoni tofauti tofauti.

Aidha, aliwaomba wakristo kuunga mkono kazi wanaofanya viongozi hasa mwakilishi wa wadi ya Gesima na kuacha kupiga domo kila wakati kwa kuwa huo si mfano mwema kama wakristo.

“Sisi kama wakristo tunastahili kuunga mkono kazi ya viongozi wetu kwa yale wametufanyia na kuwaombea mema kila wakati ili Mungu awajalie na kutenda mengi zaidi,” alihoji Mosati.

Kwingineko, amewaomba wakristo kuweka tafouti zao kando na kushirikiana pamoja ili kuinua viwango vya maendeleio mahali wanamoishi.

Mosoti alichukua fursa hiyo na kuwaomba walimu na wazazi wa shule ya Msingi na ile ya upili ya Matutu kushirikiana vyema ilio kuinua viwango vya masomo katika shule hizo.

“Walimu na wazazi wakishirikiana kwa kweli viwango vya masomo vitanawili,kwa hivyo nawaomba wazazi na walimu wetu kushirikiana  tuinue viwango hivyo,” aliongezea Mosoti.