Wakazi wote wa kaunti ya Kisii wameombwa kudumisha na kulinda mila na utamaduni wao kama njia moja ya kukumbuka mambo yanayofanyika.
Akiwahutubia wanahabari katika jingo moja la utamaduni lililoko Karibu na Shule ya upili ya Kisii, mwenyekiti wa wazee na utamaduni wa Kisii Mzee James Matundura aliwaomba wakazi wote kudumisha na kulinda utamaduni wao.
Aidha,aliwaomba viongozi wote wa Kisii kuungana pamoja na kuendeleza miradi mbali mbali ambayo itainua jamiii na kuweka tafouti zao kando ili kufanya maendeleo kwa wananchi waliowachagua.
“Nawaomba viongozi wote kuungana pamoja na kuendeleza miradi mbali mbali katika kaunti yetu hasa sekta ya kitamaduni,” alihoji mzee Matundura
Kulingana na Mzee huyo, Kaunti ya Kisii inastahili kuwa na kivutio cha watalii na vifaa vya utamaduni viwe huko, ili sekta ya utalii inawiri katika kaunti ya Kisii.
Kwingineko, aalimpongeza Gavana wa kaunti ya Kisii kwa Juhudi anazofanya za kuinua viwango vya utamaduni, hasa baada ya Ongwae kumkabidhi Rais kifaa cha utamaduni wa Abagusii, wakati wa kongamano la magavana wiki iliyopita.
Matundura amelipongeza bunge la Kaunti ya Kisii kwa kupitisha mswada wa kaunti kuwa na bendera yake ambayo iko na nembo za kitamaduni, kama mdwara amhao unaonyesha umoja wa jamii ya wakisii.
“Napongeza bunge letu la kaunti la Kisii kwa kupitisha mswada wa kuwa na bendera ya kaunti na kuweka nembo za kitamaduni katika bendera hiyo kuashiria kuwa wanapenda kaunti yao,” aliongezea Matundura.