Kamati imeundwa katika Kaunti ya Nyamira ambayo itatengeneza mswada wa kutaka Sekta ya Afya kusimamiwa na uongozi wa Kaunti hiyo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea na Mwandishi wa Habari huyu siku ya Jumatatu, Mkuu wa mafunzo katika Sekta ya Afya Kaunti ya Nyamira Charles Mogaka alisema kuwa wanataka mswada utengenezwe na kuwasilishwa kwa Bunge la Kaunti hiyo ili kupitishwa kuwa sheria.

“Tumekuwa tukifanya masuala ya usafi tukitumia sheria ya zamani ambazo zilioko chini ya uongozi wa Serikali Kuu, ndio maana tunahitaji kutengeneza sheria ambazo zitakuwa chini ya uongozi wa Serikali ya Kaunti yetu ya Nyamira,” alihoji Mogaka.

Mogaka aliongezea kuwa ongozi ukiwa chini ya Serikali ya Kaunti basi Maafisa wa Afya katika Kaunti hiyo watapata fursa ya kusimamamia afya wenyewe na hiyo itawakabidhi Maafisa hao nguvu ya kuendesha shughuli za afya katika Kaunti hiyo,” Mogaka.

Kamati hiyo ambayo imeundwa imejumuisha Maafisa kutoka sekta mbali mbali kama ile ya Afya, Kilimo, Elimu na nyinginezo ambapo mswada huo ukipitishwa na Bunge la Kaunti hiyo kuwa sheria basi Maafisa wa Afya katika Kaunti hiyo watakuwa wakisimamia shughuli zote za afya na kuimarisha afya kwa wote kwa ujumla.

Aidha, mipango yote imefanywa kikamilifu kwa kutengeneza mswada huo na baadaye kibarua kitakuwa kwa Wawakilishi wa Wadi katika Bunge la Kaunti ya Nyamira kuupitisha mswada huo rasmi kuwa sheria ambayo itawasaidia wananchi kufaidika. Haya ni kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Afya Kaunti ya Nyamira Charles Mogaka.