Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Makocha wa riadha humu nchini wanadai kuwa ongezeko la matumizi ya dawa za kuongeza nguvu miongoni mwa wanariadha nchini linachangiwa na baadhi ya makocha wa kigeni.

Makocha hao wanataka wanariadha wa humu nchini kujihadhari na makocha kama hao.

Kulingana na makocha hao ni kwamba baadhi ya wakufunzi wakigeni katika riadha hawana nia njema na ufanisi wa riadha nchini hivyo basi wanaweza wakatumiwa kwa urahisi kuharibu sifa ya Kenya katika riadha ulimwenguni.

Kwenye kikao na wana habari mjini Eldoret Jumatatu makocha hao chini ya kampuni ya Rosa & Associate ambayo hudhamini wanariadha walitaka kubuniwa kwa sera ambayo italinda wanariadha wa humu nchini dhidi ya makocha wa kigeni ambao huwatumia vibaya wanariadha wa Kenya.

Wakiongozwa na kocha Francis Mwaniki wa kambi ya riadha ya Nyahururu chini ya kampuni ya Rosa walitetea kambi ya Rosa mjini Eldoret dhidi ya tuhuma za matumizi ya dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha wake.

Mwaniki alisema wale ambao wanadai kuwa kambi hiyo inawapa wanariadha dawa za kulevya ni maadui ya kambi hiyo ambao wanatumia swala hilo dhidi ya kambi hiyo kujitakia makuu.

“Miaka yote ambayo nimekuwa kocha kambi ya Rosa haijawahijihusisha na dawa za kuongeza nguvu, wale ambao wanalaumu kambi hii kuhusiana na dawa hizo ni maadui wa kambi hii” alisema

Makocha wengine ambao walikuwa na msimamo sawa na huo ni Erick Kimaiyo, Paul Kemei, Alex Olotiptip, Chemalany Stephen, David Leting miongoni mwa wengine.

Wakufunzi hao walitaka madaktari wa wanariadha wawe madaktari amboa wanafahamu sheria za dawa za kusisimua misuli ili wasijewakawapa wanariadha dawa ambazo zimeorodheshwa kama dawa za kusisimua misuli

Kambi hiyo imekuwa ikituhumiwa kuhusiana na dawa hizo hasa baada wanariadha kutoka kambi hiyop kuadhibiwa baada ya kupatikana na hatia ya matumizi ya dawa za kulevya.

Miongoni mwa wana riadha kutoka katika kambi hiyo ambao wamenaswa katika mtego wa kutumia dawa za kulevya ni Rita Jeptoo, Mathew Kisorio na Agatha Jeruto.

Kambi ya Rosa imekuwepo kwa miaka 25 iliopita ikiwa na kambi zipatazo 8 ambazo hutoa mafunzo kwa wanariadha chini makocha wa humu nchini.

Miongoni mwa kambi hizo ni kambi ya Kaptagat, Kapsabet, Nyahururu, Kapsait, Londiani, Ngong, Mt Elgon na Kaptabuk.