Wakaazi wa kaunti ya Nakuru wametakiwa kutochokulia kwamba utunzi wa mazingira ni upanzi wa miti tu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanaharakati wa mazingira Charles Mwangi anasema kuwa ni vyema wananchi wafahamu kwamba utunzi wa mazingira huanzia nyumbani. 

"Kutunza mazingira si kupanda tu miti, bali pia ni kuweka viwango vya juu vya usafi hata katika mitaa tunamoishi," alisema Mwangi.

Mwenyekiti huyo wa Manyani Environmental Youth Group anasema kuwa iwapo viwango vya usafi vitazingatiwa basi magonjwa ambukizi yatapunguzwa. 

Ni matamshi yaliyoungwa mkono na Martin Lunalo kutoka muungano wa wakaazi eneo hilo. 

Lunalo anasema kuwa wengi wa wakaazi wanakosa kuchukulia kwa uzito swala la usafi.