Share news tips with us here at Hivisasa

Bunge la kaunti ya Nakuru limepitisha mswada maalumu wa wale wanaoishi na changamoto za ulemavu katika kaunti ya Nakuru na sasa unasubiri kutiwa sahihi na Gavana Kinuthia Mbugua kuwa sheria.

Spika wa kaunti ya Nakuru Susan Kihika alisema kuwa mswada huo ni wa umuhimu sana kwani utasaidia kulinda haki za wanaoishi na changamoto za ulemavu.

"Ningependa kuwapongeza wanachama wa bunge hili kwa kupitisha mswada huo muhimu katika maisha na maslahi ya walemavu katika Kaunti ya Nakuru,"Kihika alisema.

Naye mwakilishi wa walemavu katika bunge la kaunti ya Nakuru Emmah Mbugua alisema kuwa ni jambo la busara kwamba mswada huo ulipitishwa.

"Tulishapitisha mswada wa walemavu na natumai Gavana atautia sahihi kuwa sheria wakati wowote ili kusaidia kulinda haki za walemavu na ningependa kuwarai wanaoishi na changamoto za ulemavu kujitokeza katika afisi husika ili kupata maelezo kuhusu swala hili"akasema Mbugua.